Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:25

Watu 10,000 wakimbia mashambulizi mapya ya wanamgambo wa kiislamu nchini Msumbiji


Watu waliohama makazi yao kutoka jamii ya Impire katika mkoa wa Cabo Delgado wakimbia mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha, June 14, 2022. Picha ya AFP
Watu waliohama makazi yao kutoka jamii ya Impire katika mkoa wa Cabo Delgado wakimbia mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha, June 14, 2022. Picha ya AFP

Watu 7 waliuawa katika msururu wa machafuko yanayohusishwa na wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa Msumbiji, vyanzo vya ndani vimesema Jumanne, huku Umoja wa mataifa ukisema watu 10,000 walihama makazi yao.

Mashambulizi yalifanyika katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado, ambako wanamgambo wa kiislamu walianzisha uasi mbaya mwaka wa 2017, na kuchochea uingiliaji kati wa majeshi ya kikanda mwaka jana ambayo yalirejesha hali ya usalama.

Watu wanne walikatwa vichwa katika kijiji cha mbali cha Natupile, wakazi waliokimbia eneo hilo kwa hofu waliiambia AFP.

"Watu wa Natupile walichukuwa picha, kwa hiyo tunajua kilichotokea," Antonio Kalimuka aliiambia AFP kwa njia ya simu.

Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu Jumatano iliyopita, waliua wafanyakazi wawili kwenye mgodi wa graphite unaomilikiwa na kampuni ya Australia, Triton Mineral, kampuni hiyo ilisema.

Siku iliyofuata, wanajeshi wa kanda ya kusini mwa Afrika waliendesha shambulio dhidi ya wanamgambo hao katika msitu katika wilaya ya Macomia kaskazini mwa Pemba, mji mkuu wa mkoa wa Cabo Delgado.

"Wakati wa operesheni hiyo, magaidi waliuawa na wengine walipata majeraha mabaya," tume ya wanajeshi hao ilisema katika taarifa.

XS
SM
MD
LG