Wapiganaji kutoka kabila la walio wachache la Karen wiki iliyopita waliiteka ngome ya mwisho ya jeshi la Myanmar ndani na kuzunguka Myawaddy, ambayo imeungana na Thailand kwa madaraja mawili katika Mto Moei.
Mapigano ya karibuni kabisa yalizuka asubuhi wakati wapiganaji wa msituni wa Karen walipoanzisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Myanmar waliokuwa wamejificha karibu na daraja la pili la urafiki la Thailand na Myanmar, kivuko kikuu cha biashara na Thailand, alisema mkuu wa polisi Pittayakorn Phetcharat katika wilaya ya Mae Sot nchini Thailand.
Alikadiria kuwa akriban watu 1,300 walikimbilia Thailand.
Forum