Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:17

Watoto milioni 100 barani Afrika hawakamilishi elimu yao-Kikwete


Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati alipohudhuria sherehe za kuapishwa rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.
Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati alipohudhuria sherehe za kuapishwa rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.

Umoja wa Mataifa unapanga kuandaa mkutano mkuu mwaka huu unaohusu  mada ya Kubadilisha Elimu.  Mkutano huo unalenga kutoa fursa ya kushughulikia kile maafisa wanasema ni masuala ya kimfumo ambayo yanawazuia watoto kujifunza.

Shirika moja ambalo linapigania kubadilisha mfumo wa elimu katika nchi zinazoendelea ni Global Partnership for Education (GPE), ambalo linasaidia kutafuta fedha za kutatua baadhi ya changamoto hizo.

Mwenyekiti mpya wa GPE ni rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete anasema shirika hilo linafanya kazi katika kutoa elimu bora kwa wasichana na wavulana

Rais Kikwete akizungumza na VOA amesema “suala hili la elimu kwa GPE ni muhimu na ndio kazi yetu kwa hiyo tulikuja kukutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataaifa ili kupata kuelewana zaidi na kumuonyesha utayari wetu kufaya naye kazi.”

Aliongeza kusema wamekubaliana juu ya kuweka sawa njia za kiufundi na makamu wake atafanya kazi na ofisi ya naibu katibu mkuu juu ya maandalizi hayo na maafisa wa GPE na kupanga juu ya namna ya kufanya shughuli zao. Na wanaamini mkutano huo utakuwa na mafanikio makubwa.

Mkuu huu utafanyika wakati janga la corona likiendelea kuleta shida kaztika elimu ulimwenguni. Watalaam wanasema, inaathiri kwa kiasi kikubwa kujufunza miongoni kwa wasichana na watoto walio katika mazingira hatarishi. Wanaongeza kuwa aina mpya ya virusi Omicron inazidisha athari za janga hili kwenye mifumo ya elimu kote ulimwenguni.

Kuhusu hali ya elimu katika nchi zinazoendelea alisema kwamba hali ya elimu ni mbaya hasa katika mataifa hayo ni hivi leo robo bilioni ya Watoto hawako shuleni na bahati mbaya milioni 100 kati yao ni katika bara la Afrika na hata walio shuleni hawakamilishi elimu yao.

Na hata wale wanaomaliza masomo hawajifunzi vya kutosha na Covid imefanya hali kuwa mbaya zaidi kufungwa kwa mashule kumesababisha Watoto bilioni 1.6 kukaa nje ya shule tayari tUna tatizo la robo bilioni hii inafanya hali kuwa mbaya zaidi aliongeza.

Hali nyingine aliyogusia Kikwete ni “kutokuwa na usawa kwani hapa Marekani na Ulaya shule zilifungwa na watoto waliendelea na masomo kwa njia ya mitandao lakini shule za Afrika zilipofungwa watoto hawakuwa na namna nyingine hawakuwa na masomo kabisa, hawana kompyuta wala simu za mkononi kama ilivyo huku” alisema.

Kikwete alieleza kuwa taasisi anayoongoza inatoa fesha na kufanya kazi katika kuboresha elimu na mipango hiyo inapitia kila nchi na wao wanaamua nini wanataka kufanya ila GPE haina ofisi katika kila nchi inafanya kazi kupitia taasisi mbali mbali kama vile benki ya dunia , Unicef, Unesco na taasisi nyingine mbali mbali za kimataifa na kutoa fedha kupitia taasisi hizo.

Kwa hivyo nchi zinaamua juu ya mipango gani zinahitaji ambazo wanaamini ikitekelezwa zitakuwa na fursa ya kusaidia kuboresha mfumo wa elimu na wao wanatafuta fedha kupitia wahisani alisema.

Kikwete alikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini New York kuhusu mkutano huo ujao.

XS
SM
MD
LG