Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:31

Watoto 31 wanaozaliwa kabla ya wakati waondolewa katika Hospitali ya Shifa huko Gaza

 Watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati wao waliotolewa kwenye mashine maalum katika hospitali ya Al Shifa katika mji wa Gaza wakipokea matibabu katika hospitali ya Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. Novemba 19,2023.(REUTERS)

Takriban watoto 31 wanaozaliwa kabla ya wakati wameondolewa katika Hospitali ya Shifa huko Gaza, kulingana na mamlaka ya afya ya Palestina. Watoto hao wachanga watahamishiwa kwenye vituo vya matibabu nchini Misri.

Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina lilisema kwenye mtandao wa X, kwamba leo, timu za huduma za dharura PRCS, kwa uratibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), zimefanikiwa kuwaondoa watoto 31 waliozaliwa kabla ya kabla ya wakati.

Vikosi vya Israel viliivamia hospitali hiyo wiki iliyopita kama sehemu ya operesheni zao za kijeshi dhidi ya Hamas.

Timu ya Shirika la Afya Ulimwenguni iliitembelea Shifa Jumamosi na kuripoti kwamba kulikuwa na watoto 32 wanaohitaji huduma.

Forum

XS
SM
MD
LG