Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 17:55

Watoto 2 kati ya 4 waliochomwa visu Ufaransa wamo katika 'hali mbaya'


Maua kwa ajili ya kuwatakia afueni watoto waliochomwa visu. mua yamewekwa Le Paquier park, June 8, 2023.
Maua kwa ajili ya kuwatakia afueni watoto waliochomwa visu. mua yamewekwa Le Paquier park, June 8, 2023.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametembelea familia za Watoto 4 waliochomwa visu, na ambao sasa wanaripotiwa kuwa katika hali nzuri baada ya kufanyiwa upasuaji.

Macro na mkewe Brigitte, wametembelea Watoto watatu hospitalini ambapo wanapokea matibabu baada ya shambulizi hilo la alhamisi.

Shambulizi lilitokea katika mji wa Annecy, Alpine.

Waziri mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne, amesema kwamba Watoto hao wanne, wenye umri kati ya miezi 22 na miaka 3 walifanyiwa upasuaji na wapo chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Olivier Veran, ambaye pia ni daktari kitaaluma, amesema kwamba Watoto wawili wapo katika hali ya dharura.

Watoto watatu wanatibiwa katika hospitali mjini Grenoble, Ufaransa, huku wa nne akiwa anapokea matibabu katika nchi Jirani ya Uswizi.

Watoto wawili ni raia wa Ufaransa, na wengine ni watalii kutoka Uingereza na Udachi.

Watu wazima wawili walijeruhiwa baada ya kuchomwa kisu. Mshukiwa ambaye ni mkimbizi, mwenye umri wa miaka 31, raia wa Syria amekamatwa, na anafanyiwa ukaguzi wa kiakili.

Forum

XS
SM
MD
LG