Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:35

Watetezi wa haki za mashoga Waulalamikia mswaada unaoharamisha mapenzi ya jinsia moja


Spika wa bunge Uganda Anita Annet Among akiongoza kikao wakati wa mjadala wa mswaada wa Kupinga Ushoga, ambao unapendekeza adhabu mpya kali kwa mahusiano ya jinsia moja wakati wa kikao katika majengo ya Bunge huko Kampala, Uganda Machi 21, 2023. REUTERS

Wafuasi wa haki za mashoga wamewashutumu wabunge wa Uganda kwa kupitisha mswaada ambao unasema ni kosa la jinai kwa mtu yeyote anayejitambulisha hadharani ni shoga au wa mapenzi ya jinsia moja.

Mswaada huo ambao bunge la Uganda uliupitisha Jumanne jioni kwa sauti moja tu inayoupinga, utakuwa sheria ikiwa Rais Yoweri Museveni atautia saini kama inavyotarajiwa.

Wafuasi wa haki za mashoga wanawashutumu wabunge wa Uganda kwa kupiga kura ili kufanya kuwa kosa la jinai kwa mtu yeyote anayejitambulisha hadharani kuwa ni shoga au wa mapenzi ya jinsia moja. Mswaada huo ambao bunge la Uganda uliupitisha Jumanne jioni kwa sauti moja tu inayoupinga, utakuwa sheria ikiwa Rais Yoweri Museveni atautia saini kama inavyotarajiwa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanamtaka Rais Yoweri Museveni kuzuia kile wanachokiita mswaada wa ajabu uliopitishwa Jumanne jioni.

Katika taarifa yake Tigere Chagutah, mkurugenzi wa kanda wa Amnesty International kwa Mashariki na Kusini mwa Afrika, alisema Mswaada wa Kupinga Ushoga ni sawa na shambulio kubwa kwa watu wa mapenzi ya jinsia moja - LGBTQ na unadharau katiba ya Uganda.

Adhabu katika mswaada huo ni pamoja na kifungo cha miaka 20 jela kwa kile kinachoitwa kukuza ushoga na kuajiri watoto, wakati jaribio la kufanya ushoga litapelekea kifungo cha miaka 10 jela.

Pia unatoa adhabu ya kifo kwa yeyote anayewalazimisha watoto, watu wenye ulemavu, watu wenye magonjwa ya akili na wale walio katika umri mkubwa kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Roland Ebole ni mtafiti wa kikanda wa Amnesty International anasema mswaada huo ikiwa utatiwa saini kuwa sheria utachochea hatua za kupinga ushoga

"Haieleweki sana katika suala la ukuzaji huu ni nini unaposema kukuza ushoga. Kipengele hiki kitashawishi chuki kwa watu wa jinsia moja, kitashwishi ubaguzi na itawakatisha tamaa watetezi wa haki za binadamu na mashirika yasio ya kiserikali kufanya kazi zao." alisema Ebole.

Wabunge 389 walihudhuria mjadala wa Jumanne na upitishaji wa mwisho wa mswaada huo ikiwa ni kuonyesha uungwaji mkono uliokusudiwa kuhakikisha kuwa mswaada huo haukabiliwi na hatima ya ule mswaada wa awali wa Kupinga Ushoga ambao ulifutwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa idadi ya kutosha bungeni.

Spika haraka alipiga hesabu ya wabunge ili kuhakikisha kwamba akidi imefikiwa.

Mbunge Charles Onen alijaribu kuleta ucheshi kwenye mjadala huo katika hotuba yake "mheshimiwa Spika ninapokutazama wewe na wanawake waheshimiwa katika Bunge hili hakuna sababu ya mwanamme kukimbilia mwanamme mwingine kwa ngono. Haki mheshimiwa Spika hakuna kitu kitamu na kizuri sana kwa mwanamme zaidi ya mwanamke" aliongeza Onen.

Mbunge Fox Odoi alizomewa alipokuwa akiwasilisha ripoti ya wachache iliyosema mswaada huo ulipotoshwa na sheria ya sasa ya kanuni za adhabu inatosha kushughulikia masuala yanayohusiana na ushoga.

Baada ya mjadala wa saa sita, mswaada huo hatimaye ulipitishwa huku wabunge wakiimba wimbo wa taifa katika kusherehekea.

Bunge sasa linasubiri kura ya turufu au saini ya Museveni kabla haijatupiliwa mbali au kupitishwa kuwa sheria.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Turk alitoa wito kwa Museveni Jumatano kutotia saini mswaada huo ambao aliutaja kuwa miongoni mwa miswaada mibaya zaidi ya aina yake duniani na jambo linalosikitisha sana.

XS
SM
MD
LG