Jopo la ufalme wa Sweeden katika masuala ya sayansi Jumatano limetangaza wanasayansi watatu walioshinda tuzo ya Nobel katika kemia kwa ubunifu wao wa kemia muunganiko, na matokeo ya kemikali katika viumbe hai.
Zawadi ya tuzo hiyo ni dola za kimarekani 900,000 ambazo zimekwenda sawa kwa Carolyn Bertozzi, and Barry Sharpless wa Marekani pamoja na Morten Meldal wa Denmark.
Hii ni tuzo ya pili ya Nobel katika kemia baada ya kutolewa mara ya kwanza hapo mwaka 2001.
Jopo hilo limeeleza kwamba Meldal na Sharpless kila mmoja kwa kujitegemea waliwasilisha ubunifu wa kemikali ambazo kwa sasa zinatumika kwa upana kutengeneza dawa na vifaa mbalimbali vya kitabibu pamoja na namna ya kupannga vinasaba yaani DNA.