Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 17:57

Watanzania waomboleza kifo cha Ruge Mutahaba


Juu Rugei akiwa na familia nzima ya Profesa na mama Mutahaba. Picha kwa hisani ya Nuru the Light
Juu Rugei akiwa na familia nzima ya Profesa na mama Mutahaba. Picha kwa hisani ya Nuru the Light

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group wamiliki wa Clouds Radio na TV aliaga dunia Jumanne nchini Afrika Kusini akiwa anafanyiwa matibabu, na mwili wa marehemu utawasili Dar es Salaam, nchini Tanzania siku ya Ijumaa na utazikwa mjini Bukoba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa Serikali ambao wamefika katika msiba huo.

Amesema Marehemu ndani ya Serikali amefanya kazi kubwa sana kwa kutafsiri falsafa ya viongozi wetu. "Alianza awamu ya Nne (chini Rais Mstaafu Dkt Kikwete) na awamu hii ya tano… Amefanya kazi kubwa ya kuelimisha, ametoa mchango mkubwa wakati mwingine hata wa fedha zake…”

“Jambo hili ni kubwa kwetu Watanzania, jambo hili ni kubwa kwetu ndani ya Serikali. Hivyo natoa pole kwa Watanzania wote. Nasema hivyo kwa sababu Watanzania wote tunafahamu mchango wake,” amesema Majaliwa wakati akumzungumzia marehemu Ruge.

Kufuatia kifo hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, Mheshimiwa January Makamba ameandika barua ya majonzi kueleza ukaribu wake na marehemu.

Mazishi ya Ruge

Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa #RugeMutahaba utawasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya Ijumaa (March 1/2019).

Ikiwa hivyo wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga "mpendwa wetu" siku ya Jumamosi (March 2, 2019). .

Wasanii kutokana na kuguswa na kifo cha kiongozi, mfadhili na mshauri wao Ruge wameweza kuja na wimbo wa kumuenzi na kumuombea katika safari yake ya mwisho ambao wameuita "Asante Baba". Wasanii walioimba ni pamoja na Barnaba,Lina, pipi, Ditto,Amini wengi wao waliokuwa THT Tanzania House of Talent iliyoanzishwa na Ruge.

Nani Ruge Mutahaba?

Ruge alizaliwa Brooklyn, New York, Marekani, mwaka 1970. Shule ya msingi alisomea Arusha School ( standard 1 hadi 6), kisha akahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo alipomalizia darasa la saba.

Taarifa ya vyombo vya habari imesema kuwa baada ya hapo Ruge alisoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. na baadae kurejea Marekani. Amesema :"nikaenda kusoma San Jose University California, ambako nilichukuwa BA in Marketing na pia nikawa nachukuwa BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, (kind of 2 courses at the same time.)". Baada ya hapo Ruge akarudi tena Tanzania.

Wakati Ruge yupo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, "mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, (then hapo tuka-build good friendship). "Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment," imeeleza taarifa hiyo kuhusu Ruge.

Kuzaliwa kwa kampuni ya Prime Time

Clouds FM 88.4, ikazaa pia Prime Time Promotions iliyokuwa ina deal na matamasha ya muziki kuanzia Summer Jam ambayo baadaye ikawa Fiesta. Na pia ilihusika kuleta wanamuziki wote wa nje kuanzia kina Koffi (Olomide), Wenge BCBG, Chaka Khan, Sean Kingston, Jay-Z na Beyonce, 50 Cents, Rick Ross, Buster Rhymes, Shaggy, Cabo Snoopy, Davido, na wengine wote uwajuao wa kimataifa. Ni wengi kwa kweli. Afrika Mashariki na ya Kati hakuna aliyeweza na anayeweza kuleta wanamuziki nyota wa dunia kama Prime Time.

Kuanzishwa kampuni ya kuwasimamia wasanii

Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Taarifa hiyo imeeleza kuwa "Hivyo Ruge akaona ni bora aanzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika.

Ruge amenukuliwa alisema wakati wa uhai wake : "Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo."

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Sunday Shomari, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG