Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:31

Watanzania wamuaga Kanumba


Msani mashuhuri wa Tanzania Steve Charles Kanumba akaribishwa na mashabiki mjini Kigali.
Msani mashuhuri wa Tanzania Steve Charles Kanumba akaribishwa na mashabiki mjini Kigali.

Mcheza filamu maarufu nchini Tanzania Steven Kanumba atazikwa jumatano katika makaburi ya Kinondoni, Dar-Es-Salaam

Msanii wa filamu, aliyebeba mapenzi makubwa ya watanzania na bara la Afrika, Steven Charles Kanumba aliyefikwa na mauti ghafla Aprili 7, 2012. Kufuatana na ripoti za daktari moja aliyechunguza maiti katika hospitali ya Muhimbili ni kwamba msani huyo alifariki kutokana na majeraha ya kichwa.

Mazishi ya Kanumba, yamepangwa na kuratibiwa kwa kuzingatia heshima, umaarufu, mapenzi yake kwa watu na hadhi ya kimataifa aliyonayo, hivyo imetolewa fursa ya kila mtu mwenye nafasi kujitokeza kumuaga msanii huyo ambaye ni mwanamapinduzi wa tasnia ya filamu ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.

Rais Jakaya Kikwete Jumatatu aliongoza mamia ya waombolezaji katika msiba wa msanii huyo, akisema alilazimika kusitisha ziara yake ya nje ili kuungana na wananchi wengine katika kuomboleza msiba huo. Marehemu Kanumba aliitangaza nchi ya Tanzania kupitia filamu zake mbali mbali ambazo ni maarufu katika nchi za Afrika mashariki na kati pamoja na Nigeria.

Taarifa zaidi zinasema mwili wa marehemu utachukuliwa majira ya saa mbili asubuhi jumatano, kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili kuelekea viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu kutoka kwa viongozi wa serikali pamoja na mashirika binafsi kabla ya watu wote kumuaga.

XS
SM
MD
LG