Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 17:41

Watalii watano wauwawa Ethiopia


Moja la eneo la Ethiopia bonde la Omo linavyoonekana katika picha

Maafisa wa Ethiopia wamesema shambulizi hilo lilitokea jumanne katika eneo la Afar

Watalii watano wa kigeni wameuwawa na wengine wawili wametekwa katika shambulizi kaskazini mwa Ethiopia.

Maafisa wa Ethiopia wamesema shambulizi hilo lilitokea jumanne katika eneo la Afar.

Wamesema wajerumani wawili , raia wa hungary wawili, na mmoja kutoka Austria waliuwawa katika shambulizi la ghafla wakati mbelgiji na raia mwingine kutoka taifa lingine walijeruhiwa.

Maafisa pia wanasema wajerumani wawili walikuwa sehemu ya kundi lililotembelea eneo la volcano huko Afar wakati wa uvamizi huo.

Baadhi ya watalii hao walirejea katika mji mkuu Addis Ababa siku ya jumatano akiwemo mwanaume mmoja aliyekuwa kwenye kiti cha kusukuma. Wengi waliziba sura zao wakati wakiwa wamebebwa kwenye gari la kidiplomasia.


Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG