Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 17:57

Wataalamu waeleza changamoto zinazokabili usindikaji vyakula Afrika 


Kiwanda cha kusindika nyama Uruguay.
Kiwanda cha kusindika nyama Uruguay.

Ripoti mpya ya wataalamu wa kilimo inasema mchakato wa usindikaji vyakula vibichi na kuwa bidhaa zilizokamilika umekuwa ni kawaida mno barani humo, lakini ukosefu wa ujuzi wa kiteknolojia, ufadhili na vifaa, pamoja na vikwazo vya biashara, vinadumaza maendeleo.

Kundi la watalaamu wa kilimo linasema maendeleo ya sekta ya usindikaji barani Afrika huenda ikazuia uwepo wa takataka na kupungua njaa.

Mahitaji ya Chakula

Mahitaji ya chakula ambacho kimesindikwa yameongezeka barani AFrika wakati idadi ya watu inaongezeka, inasema ripoti ya kurasa 63 kutoka kundi la watalaamu wa chakula linalojulikana kama Malabo Montpellier Panel.

Ousmane Badiane ni mwenyekiti mwenza wa jopo hilo. Ameiambia VOA kuwa kuongezeka kwa watu wa daraja la kati ambao wanataka kutumia vyakula vya Kiafrika kwa urahisi wa kisasa kama kuboresha viufngashio na kuwa na njia mbadala ya vyakula vilivyo tayari kuliwa.

Badiane anaeleza kuwa: “Mchanganyiko wa idadi ya watu inayoongezeka na kukua kwa kipato na ukuaji mijini umepelekea idadi kubwa na inayokuwa ya tabaka la daraja la kati. Kinachofurahisha kuhusu daraja la kati, ni kwamba wanataka kuendelea kula vyakula vya asili ambavyo wamekuwa navyo. Lakini wanataka kuvila kitofauti. Vikiwa katika vifungashio vizuri, vimewekwa vizuri, tayari kupikwa, tayari kula nap engine kuokoa muda mwingi na mengine mengi.”


Forna Health Foods

Moja ya vyakula hivyo ambavyo vinazalishwa na Forna Health Foods nchini Uganda. Forn inatengeneza unga, ambao unakuwa na mchanganyiko wa unga tofauti aina 12 ili kutengenea unga wa uji kwa ajili ya watoto na wazee.

Mkurugenzi wa kampuni, Hilary Beinemigisha, anasema bidhaa zao za chakula zina lishe na rahisi kutayarisha.

Bainemigisha anaeleza: “Tuna njia mbili. Tuna moja ambayo haihitaji kupikwa. Ni maarufu sana miongoni mwa watu wa maofisini, walio katika makampuni ambao wako ofisini. Ni maarufu sana miongoni mwa wasafiri, wanafunzi, watu walio katika mahospitali ambao hawana uwezo wa kuwa na fursa ya maji ya moto kwenye chupa. Lakini hata kwa kupika, mtu anasema kuwa na njia ya kupika, unahitaji kuchemsha maji au maziwa mpaka yachemke halafu unaongeza mchanganyiko na kuukoroga.”

Lakini Bainemigisha anasema kampuni yake inakabiliwa na vikwazo, kama vile fursa ya upatikanaji wa chakula kibichi cha kutosha nje ya msimu wa mavuno.

Kwasababu ya hilo, Bainemigisha anasema kutengenea chakula kizuri kwa bei nafuu nayo si kazi rahisi.

Bei za Nafaka Ziko Juu

Mkurugenzi huyo anaongeza kuwa: “Mbali na msimu wa mavuno, bei za nafaka ziko juu. Lakini kwetu sisi, bidhaa lazima zibaki katika bei zile zile. Kwahiyo, faida yetu inapungua kwa kiasi kikubwa sana mbali na mavuno. Lakini wakati wa mavuno, faida yetu inakuwa nzuri. Pili, tunachanganya unga aina nyingi na hiyo ina maana gharama za uzalishaji wetu zinakuwa juu.”

Sekta ya usindikaji chakula pia inakabiliwa na changamoto kutokana na uksoefu wa miundo mbinu na uendeshaji wa vifaa. Idara ya Umoja wa Mataia ya Chakula na Kilimo inasema asilimia 30 mpaka 40 yc hakula kinachozalishwa barani Afrika kinapotea kabla ya kumfikia mteja. Kupotea kwa chakula au kiwango cha hasara kinakadiriwa kuwa dola trilioni moja kila mwaka.

Wataalamu wa Kilimo

Watalaamu wa kilimo wanazilaumu serikali za Afrika kwa kushindwa kulinda uvumbuzi wa teknolojia ambayo kazi yake inanakiliwa na kuibwa, ambayo imepelekea baadhi kujiondoa katika biashara barani Afrika.

Badiane anasema sekta ya usindikaji ni muhimu katika kuendeleza maeneo ya vijijini na inahitaji mtizamo wa serikali.

Badiane anatoa maelezo zaidi: “Haya ni mazingira yanayohusu kuibuka kwa sekta ya usindikaji, ambayo nadhani katika nyakati nyingi haijafikia kiwango cha mtizamo ambao kinahitaji kutoka serikalini. Lakini hili ni jambo muhimu sana linalofuata katika kuendeleza na kuboresha maeneo ya vijijini. Ni ajabu, ni mbali sana kutoka maeneo ya vijijini. Bado hawajatengeneza kiungo hicho. Nadhani ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.”

Watafiti wanasema Ghana, Kenya, Senegal na Afrika Kusini wamepata maendeleo katika kushawishi ukuaji wa makampuni ya usindikaji chakula.

wanasema nchi hizo zimeweka usalama wa chakula na udhibiti wa ubora, zimewekeza katika teknolojia na elimu ya ufundi na mafunzo, na kutoa afueni ya kodi, na kuhakikisha usambazaji wa mali ghafi, na kutoa fursa ya mikopo ya kifedha, ambayo inasaidia usindikaji unaohitajika kwa kununua mashine bora na kuboresha uwezo wa uzalishaji.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Mohammed Yusuf, Nairobi.

Forum

XS
SM
MD
LG