Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:28

Uhispania, Mauritania na Gambia zasaini mikataba ya kuhalalisha uhamiaji

Picha hii inaonyesha boti iliyokuwa inasafirisha wahamiaji kutoka Afrika ikiwasili kwenye bandari ya kisiwa cha Canary, Uhispania, Agosti 24, 2024. Picha ya AFP
Picha hii inaonyesha boti iliyokuwa inasafirisha wahamiaji kutoka Afrika ikiwasili kwenye bandari ya kisiwa cha Canary, Uhispania, Agosti 24, 2024. Picha ya AFP

Uhispania ilisaini mikataba na Mauritania na Gambia kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu na kudumisha uhamiaji halali.

Uhispania ilisaini mikataba na Mauritania na Gambia kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu na kudumisha uhamiaji halali.

Waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez anazuru eneo hilo la Afrika Magharibi kutokana na kuongezeka kwa wahamiaji wanaowasili nchini humo.

Uhispania ilisaini mkataba wa maelewano kuhusu “uhamiaji wa mzunguko” na Mauritania Jumanne na Gambia Jumatano.

Mikataba hiyo inaweka mfumo wa kuingia mara kwa mara Uhispania kulingana na mahitaji ya wafanyakazi, na msisitizo kwa vijana na wanawake.

Sanchez aliwasili katika mji mkuu wa Senegal Dakar Jumatano jioni kwa siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake, akihudhuria hafla ya maonyesho ya miradi ya ushirikiano kwenye taasisi ya Uhispania ya Cervantes.

“Tunataka kuwa karibu kama marafiki na washirika, kufanya kazi pamoja katika kila sekta ambazo ni muhimu sana kwa jamii zetu mbili,” Sanchez alisema wakati wa hafla hiyo.

Kiongozi huyo wa Uhispania anatarajiwa kukutana na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye leo Alhamisi.

Forum

XS
SM
MD
LG