Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:58

Wataalam wathibitisha zipo athari za mabadiliko ya tabia nchi Marekani- Ripoti


Athari ya moto ulioteketeza makazi California
Athari ya moto ulioteketeza makazi California

Ripoti moja ya Serikal ya Marekani inasema kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo mvua kubwa, ukame na moto katika misitu imeendelea kuongezeka nchini Marekani.

Ripoti hiyo, iliyo andikwa kwa msaada wa zaidi ya dazeni ya wakala za serikali ya Marekani na idara zake, mara kadhaa inakinzana na matamko na sera za Rais wa Marekani Donald Trump.

Ripoti iliyopitishwa na Bunge la Marekani ilitolewa kimya kimya siku ya Ijumaa wakati wa sikukuu mwisho mwa wiki.

Baadae White House iliipuuza ripoti hiyo kwa kusema siyo sahihi, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la habari la Reuters.

Msemaji wa White House Lindsay Walters ameiambia Reuters Ijumaa kuwa ripoti hiyo ilikuwa imejikita zaidi katika hali mbaya zaidi, ambayo inapingana na matukio ya muda mrefu ya dhana ya kwamba… hakutakuwa na teknolojia na ubunifu wa kutosha, na ongezeko la haraka la watu.

Tathmini hiyo ya hali ya hewa ya Taifa, iliokuwa na zaidi ya kurasa 1,000, imetahadharisha kuwa maafa makubwa na ya muda mrefu yanayotokana na hali ya hewa kwa uchache kwa upande fulani yatasababishwa na kuongezeka kwa joto duniani.

Imesema kuwa maafa ya hali ya hewa yanageuka kuwa ni vitu vya kawaida nchini na kutahadharisha kuwa bila ya hatua madhubuti hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi.

XS
SM
MD
LG