Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:12

Wasomali wajadili uthabiti wa nchi yao


Polisi na wanajeshi wakikusanyika kwenye eneo lililotokea mlipuko wa kujitoa mhanga karibu na makazi ya rais wa Somalia, Sheikh Sharrif Sheikh Ahmed mjini Mogadishu, March 14, 2012
Polisi na wanajeshi wakikusanyika kwenye eneo lililotokea mlipuko wa kujitoa mhanga karibu na makazi ya rais wa Somalia, Sheikh Sharrif Sheikh Ahmed mjini Mogadishu, March 14, 2012

Rais wa Somalia, Sheikh Shariff Ahmed na Waziri Mkuu wake Abdiweli Mohamed Ali ni miongoni mwa washiriki wa mkutano unaofanyika Ethiopia ili kutafuta suluhisho nchini Somalia

Viongozi wa makundi ya kisiasa yanayopingana nchini Somalia wanakutana na wapatanishi wa kimataifa kujadili masuala muhimu yanayozuia kuundwa kwa serikali itakayoshika madaraka baada ya serikali ya mpito kufunga shughuli zake.

Mkutano huo unafanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa siku mbili. Rais wa Somalia, Sheikh Shariff Ahmed anahudhuria mkutano huo pamoja na Waziri Mkuu, Abdiweli Mohamed Ali, kadhalika spika wa bunge na rais wa eneo lililojitenga la Puntland. Pia kuna wajumbe maalum wa vyama vingine wanotarajia kuwasaidia wanasiasa hao kumaliza sifa mbaya ya Somalia ya kuwa mojawapo ya mataifa yaliyoshindwa kabisa kuwa na uthabiti wa kiutawala.

Licha ya sura zenye tabasamu na kupokezana mikono washiriki wanajua kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa kufuatia mpango uliokubaliwa kimataifa wa kuwepo na serikali inayofanya kazi ifikapo hapo Agosti 20.


Mjumbe mmoja alisema njia ya kufikia lengo hilo ni kama barabara iliotandwa na milipuko. Kuna masuala mengi tete. Miongoni mwake ni kuchaguliwa kwa kundi la baraza la wazee 825 kutoka koo mbalimbali zinazozozana ambao wataidhinisha katiba na kuchagua wanachama wa bunge litakalochukuwa mamlaka baada ya serikali ya mpito.

Ratiba inataka bunge kuwa tayari ifikapo Juni 15. Na huku zikisalia siku 90 awamu ya serikali ya mpito imalizike vyama vyote vinajibidiisha kumaliza tofauti baina yao.




XS
SM
MD
LG