Mkutano huo wa 29 wa marais na viongozi wa AU ulifunguliwa rasmi Jumatatu mjini Addis Ababa, Ethiopia.
“Hali ilivyo Sudan Kusini, Somalia, Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati, mahusiano yaliyotetereka kati ya Djibouti na Eritrea, matatizo ya kuleta mwafaka wa amani Mali, ambako ugaidi wa kidini unaendelea, hali ya kisiasa kati baadhi ya nchi za Afrika, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Guinea-Bissau, yanatosha kuthibitisha wasiwasi huu.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aliwasilisha mchango wa dola za marekani milioni 1 kwa Umoja wa Afrika katika hatua za kukifanya chombo hicho kiwe sio tegemezi.
Takriban asilimia 60 ya bajeti ya Umoja wa Afrika inatokana na misaada ya kigeni, ikiwemo Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia na nchi ambazo sio wanachama.
Bajeti ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2017 ni dola milioni 782. Julai 2016, viongozi wa Umoja wa Afrika walikubaliana kuweka ushuru wa asilimia 0.2 kwa baadhi ya bidhaa zinazoingia Afrika katika juhudi ya kufidia gharama za matumizi yao.
Mkutano huo wa siku mbili utajikita katika maudhui ya kuwekeza kwa ajili ya ajira za vijana.