Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:29

Msichana mwengine wa Chibok, Nigeria aokolewa


Msichana wa shule ya Chibok Amina Ali aliyeokolewa kutoka Damboa.
Msichana wa shule ya Chibok Amina Ali aliyeokolewa kutoka Damboa.

Jeshi la Nigeria linaeleza kwamba msichana wa pili kati ya wasichana wa shule waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram miaka miwili iliyopita ameokolewa.

Msemaji wa jeshi, Kanali Sani Usman, alisema kupitia barua pepe kwamba jina la msichana huyo ni Serah Luka, na kuongeza kwamba alikuwa mwenyeji wa kijiji cha Madagali katika jimbo la Adamawa.

Jeshi lilitoa picha yake, akiwa amevalia buibui sawa na iliyovaliwa na wasichana waliotekwa na ambao wamekuwa wakionekana kwenye video za Boko Haram.

Serah ni wa pili kuokolewa kati ya wasichana 219 waliotekwa na kuendelea kushikiliwa na kundi la Boko Haramu tangu mwaka wa 2014.

Siku ya Alhamisi, msichana mwenye umri wa miaka 19, Amina Ali, aliokolewa na raia kutoka kwa msitu wa Sambisa, katika jimbo la Borno, akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miezi minne. Msichana huyo anaendelea kuhojiwa na maafisa wa kijeshi wa Nigeria.

XS
SM
MD
LG