Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 02:41

Washukiwa wanne wa Al-Shabaab wauawa na Jeshi la Kenya


Wanajeshi wa Kenya wakifanya mazoezi ya kivita katika mafunzo yanayotolewa na Jeshi la Uingereza, Machi 26, 2018.

Wanajeshi wa Kenya Alhamisi wamewaua washukiwa wanne wa wapiganaji wa kikundi cha Al-Shabaab na kumkamata mmoja wao baada ya tukio la kushambuliwa basi katika Kaunti ya Lamu.

Mratibu wa Mkoa wa Pwani John Elungata ametoa ripoti hiyo masaa kadhaa baada ya shambulio la kushitukiza katika eneo la Nyongoro, sehemu maarufu ambayo Al-Shabaab imekuwa ikifanya mashambulizi yanayo lenga abiria katika magari na vyombo vya usalama.

Watu watatu waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya sana wakati washukiwa wa wapiganaji wa Al-Shabaab waliposhambulia basi lililokuwa linaelekea Lamu kutoka Mombasa.

Magaidi hao imefahamika kuwa walikuwa wanajaribu kulazimisha basi lisimame lakini dereva aliongeza mwendo, na hivyo ikawafanya walirushie basi hilo risasi.

Kamishna wa Kaunti Irungu Macharia amesema wale waliouawa na wengine waliojeruhiwa hawajaweza kutambuliwa hadi hivi sasa.

Timu za maafisa usalama zilipelekwa katika eneo la Nyongoro na maeneo yanayo lizunguka ili kukabiliana na wale waliowashambulia watu hao kwa bunduki.

Shughuli za usafiri zilisitishwa katika barabara ya Lamu-Garsen baada ya mabasi yaliyokuwa yanaelekea Mombasa kutoka Lamu na yale yanayo toka Lamu kwenda Mombasa yalilazimishwa kurudi Kituo cha Polisi cha Witu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG