Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 19:34

Washukiwa 13 wakamatwa Ethiopia kutokana na mauwaji ya mwanasiasa wa upinzani


Wanajeshi wa Ethiopia wakishika doria kufuatia ghasia nchini, na hasa kwenye mkoa wa Oromia. Picha ya maktaba
Wanajeshi wa Ethiopia wakishika doria kufuatia ghasia nchini, na hasa kwenye mkoa wa Oromia. Picha ya maktaba

Polisi nchini Ethiopia wamewakamata washukiwa 13 juu ya mauwaji ya kiongozi maarufu wa upinzani kutoka jimbo la Oromia, chombo cha habari cha ndani kimesema.

Mwili wa Bate Urgessa kutoka chama cha Oromo Liberation Front, OLF, ulipatikana Jumatano ukiwa umetupwa karibu na barabara nje ya mji wa Meki, muda mfupi baada ya kukamatwa na wanajeshi wa serikali, chama chake kimesema.

Marekani, Umoja wa Ulaya na Uingereza wameungana na wanaharakati wa haki za binadamu kutaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na mauaji ya Bate, ambaye alikuwa mwanasiaa muwazi, na ambaye kwa miaka mingi alikuwa akiwekwa kizuizini na kutolewa.

Polisi kutoka eneo la East Shawa ambako mwili wake ulipatikana wamewakamata washukiwa 13 kutokana ufyatuaji risasi, mtandao wa utangazaji wa Oromia umesema Alhamisi, ukiongeza kuwa Bate alizikwa Alhamisi mjini humo.

Bate mwenye umri wa miaka 41 aliachiliwa kwa dhamana mapema mwezi uliopita baada ya kukamatwa akiwa na mwanahabari wa Ufaransa Anatoine Galindo, baada ya kukamatwa Februari.

Forum

XS
SM
MD
LG