Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:20

Washirika wagawanyika juu ya azma ya Russia


Watu wakishiriki katika matembezi ya mshikamano, kuonyesha moyo wa uzalendo wa wananchi wa Ukraine wakati mvutano na Russia ukiongezeka, huko Kyiv, Ukraine, Feb. 12, 2022.
Watu wakishiriki katika matembezi ya mshikamano, kuonyesha moyo wa uzalendo wa wananchi wa Ukraine wakati mvutano na Russia ukiongezeka, huko Kyiv, Ukraine, Feb. 12, 2022.

Mchezo wa kubuni kuhusu azma ya Rais wa Russia Vladimir Putin uliendelea Jumapili, huku maafisa wa jeshi wa nchi za Magharibi na wataalam huru waliokuwa na mashtuko wakikubaliana kuwa Kremlin imeweka vikosi vya kutosha kuivamia Ukraine.

Lakini kutokubaliana kunaendelea kati ya washirika iwapo mkusanyiko wa jeshi hilo ni mbinu iliyotumika ni mpango wa kutaka kupata ridhaa kutoka Magharibi au ni maandalizi ya uvamizi wa jeshi.

Washington na London zinaamini Russia siyo inajidai tu, na kwamba majeshi yaliyopelekwa sehemu tatu za Ukraine siyo tu kuonyesha uwezo wa kuvamia lakini yako tayari kutekeleza shambulizi.

“Kitu kinacholeta wasiwasi ni kwamba licha ya kuongezeka kwa harakati za kidiplomasia, ongezeko la wanajeshi limendelea. Hawajasitisha, hali hiyo imeendelea,” Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema Jumamosi.

Wallace alifananisha diplomasia ya Magharibi iliyokusudia kuepusha uvamizi wa Russiakwa Ukraine ni kuwaridhisha, akiyaambia magazeti huko London kuwa “kuwepo dalili ya lililotokea Munich kwa baadhi ya watu Magharibi,” akikumbushia makubaliano ya Munich mwaka 1938 ambayo yaliruhusu vikosi vya Nazi vya Ujerumani kujiingiza Sudentenland huko Czechslovakia.

Licha ya mazungumzo ya Wallace, bendera ya Uingereza ilishushwa Jumapili katika ubalozi wake mjini Kyiv, huku wafanyakazi raia wa nchi hiyo wakisema wameambiwa ubalozi utafungwa rasmi Jumatatu, huku balozi na waambata wa kijeshi wakibakia nchini.

Wakati maafisa wa Uingereza wakihofia Putin yuko tayari kupuuzia vitisho vya vikwazo vya Magharibi na tayari amevitathmini katika hisabu yake ya kivita, wenzao wa Paris na Berlin wanaamini kuongezeka kwa tishio hakutatokea wiki hii.

Maafisa wa Ufaransa wanaipa uzito mdogo ripoti ndefu ya kipelelezi kutoka Pentagon na mashirika ya kipelelezi ya Marekani, ambao walishirikiana na washirika wa NATO, wakielezea mpango mzima wa uvamizi wa Russia unaoaminika umepangwa kufanyika Jumatano hii.

Putin na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron walifanya mazungumzo ya saa mbili Jumamosi. Afisa wa ikulu ya Elysee aliviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa Putin hakutaja “dishara yoyote ya kuwa nchi yake itafanya uvamizi.”

Maafisa wa Ufaransa bado wana matumaini kuwa diplomasia inaweza kuepusha mzozo, wanasema Putin na Macron wamekubaliana kkuwa na majadiliano zaidi, kama ilivyo kwa Rais wa Marekani Joe Biden na kiongozi wa Russia wamekubaliana kufanya hivyo wakati wa mazungumzo yao ya saa nzima Jumamosi.

XS
SM
MD
LG