Hali hiyo imezusha wasiwasi mpya kuhusu uhalifu unaofanyika katika mkoa huo baada ya pande zinazohasimiana kutia saini makubaliano ya amani zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Wanadiplomasia na wataalamu wengine walitarajia kwamba mkataba huo ungekomesha mateso katika mkoa huo wenye takriban watu milioni tano ingawa usambazaji wa misaada umeanza tena baada ya Novemba 2 kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Afrika kusini.
Wanajeshi wa Eritrea jirani na Ethiopia katika mji wa Amhara ambao wamekuwa wakipigana upande wa jeshi la serikali la Ethiopia katika mzozo wa Tigray wamepora biashara , mali binafsi, na zahati za afya huko Shire mji wa kaskazinimagharibi ambao ulichukuliwa na wapiganaji wa Tigray mwezi uliopita , wafanyakazi wawili wa msaada wameliambia shirika la habari la AP .
Wamedai kutotambulishwa kutokana na sababu za kiusalama. Vijana kadhaa wametekwa na vikosi vya Eritrea kwenye mji wa Shire , wafanyakazi wa msaada wamesema.
Mmoja alisema aliona zaidi ya vijana 300 wakikusanywa na wanajeshi wa Ehiopia katika ukamataji wa pamoja baada ya mji wa Shire kukamatwa ambao ni eneo la watu wengi waliokoseshwa mkazi ndani ya nchi.