Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 17, 2021 Local time: 10:23

Tuzo za Nobel zatangazwa.


Picha za wanasayansi waliotangazwa kushinda tuzo za kwanza za Nobel mwaka huu.

Tuzo za kwanza za Nobel za mwaka huu zimetangazwa na Kamati ya Nobel ilioko Stockholm ambayo imewatuza wanasayansi kutoka Ireland, Japan na China kwa uvumbuzi wa dawa.

William Campbell kutoka Ireland na mwenzake Satoshi Omura kutoka Japan wamegawana zawadi moja kwa matibabu maarufu kama 'Novel Therapy' dhidi ya uambukizaji unaosababishwa na minyoo. Tu You-you kutoka China naye aligundua dawa ambayo imepunguza pakubwa idadi ya vifo vya wagonjwa wa malaria.

Campbell kwa sasa ni mtafiti katika chuo kikuu cha Drew kilichoko Madison kwenye jimbo la New Jersey. Omura naye kwa upande wake ni Profesa katika chuo kikuu cha Kitasato kilichoko Japan huku Tu, akiwa profesa mkuu kwenye chuo cha madawa ya kijenyeji nchini China.

Ona maoni (1)

mjadala huu umefungwa
XS
SM
MD
LG