Mauaji hayo yametokea wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani na mawaziri wengine wa mambo ya nje kutoka nchi za kiarabu wakifanya ziara nchini humo kwa ajili ya mkutano wa kilele.
Hakuna kundi lililodai kuhusika katika ufyatuaji huo wa risasi katika mji wa Hadera, ulioko umbali wa kilomita 50 kaskazini mwa Tel Aviv.
Tukio hilo linajiri siku 5 baada ya raia mmoja muarabu wa Israel kuua watu wanne kwa kuwachoma kisu katika mji wa kusini wa Beersheba, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na mpita njia.
Video ya kamera ya ulinzi iliyopeperushwa kwenye vituo vya televisheni vya Israel imeonyesha watu wawili wakifyatua risasi na bunduki za kushambulia kwenye barabara kuu ya Hadera.