Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 08:02

Wasafirisha dawa za kulevya waandaliwa kunyongwa


Wasafirisha dawa za kulevya wawili, raia wa Australia, walichukuliwa kutoka katika gereza la Bali, mpaka kwenye kisiwa watakapo nyongwa, huko nchini Indonesia.

Pamoja na raia hao wa Australia, Andrew Chan (31), na Myuran Sukumaran (33), kuna raia wa Nigeria aliyezaliwa Hispania, pia alisafirishwa kwenye kisiwa kilicho nje ya kisiwa kikuu cha Indonesia, cha Java.

Wanageria wawili, mwanamke wa kifilipino na wanaume wanne raia wa Brazil, Mfaransa na raia wa Ghana na Indonesia pia wamepangwa kunyongwa.

Hakuna tarifa hadi sasa ni wangapi wamepelekwa kwenye kisiwa cha Nasakambangan, ambako wanatarajia kupigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha siku zijazo.

Chan, na Sukumaran, walipewa jina la viongozi wa “Bali Nine,” kundi la Waaustralia, tisa waliokamatwa katika uwanja wa ndege wa Bali, mwaka 2005.

XS
SM
MD
LG