Warsha kuhusu vijana na nafasi za kazi ilifanyika mjini Nairobi wiki hii ikilenga mbinu za kupunguza tatizo la ukosefu wa kazi baina ya vijana ambalo limekuwepo kwa muda mrefu katika mataifa ya Afrika Mashariki, Shirika la Vijana almaarufu Africa Youth Trust kwa ushirikiano na Plan International chini ya usimamizi wa serikali ya Kenya, limeandaa warsha hiyo ya siku mbili jijini Nairobi kuwapa vijana ujuzi wa kujiendeleza katika masuala ya biashara na uongozi. Mwandishi wetu wa Nairobi, Kennedy Wandera, alihudhuria warsha hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo.