Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:49

Warepublikan waelekea kuchukuwa udhibiti wa baraza la wawakilishi


Jengo la bunge la Marekani, mjini Washington DC.
Jengo la bunge la Marekani, mjini Washington DC.

Warepublikan Jumatatu wamesogea kupata ushindi na kudhibiti baraza la wawakilishi katika kikao cha bunge kinacho tarajiwa kuanza Januari.

Warepublikan Jumatatu wamesogea kupata ushindi na kudhibiti baraza la wawakilishi katika kikao cha bunge kinacho tarajiwa kuanza Januari.

Warepublikan tayari wameshinda viti 212 huku Wademokrat wakiwa na viti 204 ukiwa ni muelekeo wa vyama vyote kutaka kupata jumla ya viti 218 ambapo ndipo mstari wa chama kufikia udhibiti.

Lakini wachambuzi wa uchaguzi wanasema kuhesabiwa kwa kura ambapo viti 19 vilivyosalia, vinaonekana kuelekea kwa chama cha Republikan ambapo itakiwezesha kuchukuwa udhibiti ambao sasa unashikiliwa na chama cha Demokrat.

Wakati wanaohesabu kura zilizo pigwa kwa njia ya posta wakiendelea na zoezi, inaelezwa itachukuwa siku kadhaa kukamilika.

Hapo ndipo kwa chama cha Republikan kitafikia idadi ya wingi wa viti wa 218 na kuchukuwa rasmi udhibiti na uwezekano wa kutoa upinzani kwa rais wa Marekani, Joe Biden na kuanzisha uchunguzi wa makosa ya utawala wake katika kipindi cha miaka yake miwili ya mwanzo.

XS
SM
MD
LG