Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:57

WaRepublican wameungana na Democratic kupiga kura ya kumkemea Greene


Mbunge Marjorie Taylor Greene. Mrepublican anayeiwakilisha Georgia, Feb. 4, 2021.
Mbunge Marjorie Taylor Greene. Mrepublican anayeiwakilisha Georgia, Feb. 4, 2021.

Greene analalamikiwa kwa kuelezea uungaji mkono wa nadharia za njama zisizo na msingi pamoja na nadharia ya mrengo wa kulia ya QAnon ambayo inasema wa-Democratic wasomi ni washirika wa kundi linaloabudu shetani

Baraza la wawakilishi Marekani lilipiga kura Alhamisi katika azimio lililowasilishwa na wa Democrat kumkemea mbunge M-Republican ambaye alihamasisha ghasia dhidi ya wenzake kutoka chama cha Democratic.

Wa-Republican 11 waliungana na wa-Democratic kwa kupiga kura 230 kwa 199 dhidi ya mbunge Marjorie Taylor Greene baada ya kiongozi wa-Republican Kevin McCarthy alipokataa kumkemea mbunge huyo mwanamke siku ya Jumatano.

Azimio hilo linawaruhusu wabunge kumvua nafasi za kamati mbunge huyo wa muhula wa kwanza akiliwakilisha jimbo la kusini mashariki mwa Georgia. Greene analalamikiwa kwa kuelezea uungaji mkono wa nadharia kadhaa za njama zisizo na msingi, pamoja na nadharia ya mrengo wa kulia ya QAnon ambayo inasema wa-Democratic wasomi ni washirika wa kundi linaloabudu shetani.

XS
SM
MD
LG