Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:06

Wapinzani wataka watanzania kujadili sheria ya mabadiliko ya katiba


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania wamesisitiza madai yao ya kutaka kurejeshwa bungeni muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya yenye ridhaa ya watanzania wote.

Wakizungumza katika mahojiano maalum na sauti ya Amerika-VOA viongozi hao Freeman Mbowe wa CHADEMA, James Mbatia wa NCCR MAGEUZI na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF wamesema kilichofanyika bungeni kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi-CCM kupitisha muswada huo wa sheria ya mabadiliko ya katiba kibabe kutaliweka taifa katika wakati mgumu kupata katiba bora yenye maslahi kwa watanzania wote.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wapinzani walisusia mjadala wa sheria ya mabadiliko ya katiba bungeni hivi karibuni wakiwa na madai kadhaa kubwa zaidi ni kutoshirikishwa wananchi wa upande wa Zanzibar, vipengele vya muswada huo vinavyompa madaraka makubwa Rais wakati wa upatikanaji wa wajumbe wa bunge maalum la katiba na pia kipengele kinachoivunja tume ya mabadiliko ya katiba mara tu tume hiyo inapokabidhi rasimu kwenye bunge la katiba.

Viongozi hao wa vyama vya upinzani Jumanne walikutana na wajumbe wa jukwaa la katiba na asasi nyingine zisizo za kiserikali ikiwa ni harakati za kuunganisha nguvu kupinga muswada huo ambao unasubiri saini ya Rais ili kuwa sheria.

Sauti ya Amerika-VOA imefanya mahojiano na Pindi Chana, mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:05 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Aidha vyama hivyo vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI na CUF vimeandaa mikutano ya hadhara wakianzia jijini Dar Es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha, na Kigoma ili kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kwamba mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa sasa hauko sawa na hivyo wanapaswa kushinikiza mabadiliko yenye tija kwa taifa zima.
XS
SM
MD
LG