Kuchaguliwa tena kwa Rais Cyril Ramaphosa kama kiongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini kumeimarisha madaraka yake lakini wapinzani wake wakubwa katika kamati yake mpya ya utendaji wanapendekeza kuwa mwelekeo wa nchi kuelekea kwenye mageuzi yanayohitajika sana utabakia kuwa ngumu.
Ramaphosa alichaguliwa tena, na kumfungulia njia ya kuwania muhula wa pili wa urais mwaka 2024, Jumatatu katika kura ya wanachama wa African National Congress (ANC) ambayo pia ilichagua wajumbe wapya wa mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho (NEC).
Upigaji kura huo uliwaweka kando baadhi ya mawaziri na wengine katika kambi ya kumpinga Ramaphosa ambayo ina uhusiano na Jacob Zuma ambayo, pamoja na rais huyo wa zamani aliyejiingiza katika kupambana na madai ya ufisadi ambayo anayakanusha, aliungana na waziri wa zamani wa afya Zweli Mkhize.