Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 08:38

Wapiganaji watishia viongozi na wapiga kura Cameroon


Wanajeshi wa Cameroon wanaopigana na wapiganaji

Shughuli ya kampeni imeanza nchini Cameroon, kwa ajili ya kuchagua waakilishi katika mabaraza ya majimbo, katika uchaguzi utakaofanyika Desemba 6.

Uchaguzi huo unaandaliwa wakati kuna tisho la mapigano kutoka kwa makundi yanayotaka kujitenga na kuunda nchi yao yenye watu wanaozungumza kiingereza kutoka kwa sehemu zingine za nchi zenye watu wanaozungumza kifaransa.

Mashambulizi yametokea dhidi ya maafisa waliotumwa kufanikisha uchaguzi huo huku serikali ikiendelea kutoa wito kwa raia kushirikiana na maafisa wa usalama na kutounga mkono makundi ya wapiganaj.

Emille Ngalla, mwenye umri wa miaka 47 na ambaye ni Diwani, alikimbia kutoka Bui hadi Mezam ambazo ni sehemu zinazokaliwa na watu wanaozungumza kiingereza, kaskazini magharibi mwa Cameroon.

Anasema kwambw apiganaji walienda nyumbani kwake na kutishia kumuua endapo atashiriki katika uchaguzi wa baraza la eneo hilo, utakaofanyika Desemba 6.

"Sina uhakika kama nitashiriki katika uchaguzi huo lakini kile ambacho nataka kuomba sana ni kwa serikali kuimarisha usalama kwa wale wenye ujasiri wa kupiga kura. Swala la uchaguzi linaendelea kuleta hofu kubwa sana.”

Ngalla anasema kwamba ataishi katika mji wa Bamenda, ulio kaskazini magharibi, unaokaliwa na idadi kubwa ya watu wanaozungumza kiingereza hadi uchaguzi umalizike. Anahisi kwamba mji huo ni salama.

Maafisa wa serikali katika sehemu za kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon wanasema kwamba madiwani na viongozi wa kitamaduni ambao huamua mshindi katika uchaguzi wa majimbo hayo, wanaedneela kupata vitisho dhidi ya maisha yao kutoka kwa makundi ya wapiganaji.

Wapiganaji wasambaza video kuonya wapiga kura

Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha mwanamme mwenye umri wa makamo, akitishia wagombea wanaofanya kampeni kwamba atawaua.

Anasikika akisema kwamba anajulisha jumuiya ya kimataifa kwamba uchaguzi wa desemba 6 2020 hautafanyika.

Gavana wa eneo la kaskazini magharibi mwa Cameroon Debn Tchoffo, amesema kwamba makundi ya wapiganaji yamekuwa yakipiga simu na kutishia wagombea na wapiga kura.

Amesemwa kwamba wanajeshi wametumwa eneo hilo kutoa usalama kwa piga kura, wagombea na vifaa vya kupigia kura akionya wapiganaji kwamba watauawa endapo watafanya mashambulizi.

Ametaka wapiganaji hao kujisalimisha akisisitiza kwamba uchaguzi huo utatoa fursa nzuri kwa watu wanaoishi katika maeneo yanayozungumza kiingereza kupata viongozi, namna walivyoomba wakaazi wa maeneo hayo.

Gavana huyo amesema kwamba wapiganaji walishambulia msafara wa jeshi na kujeruhi wanajeshi wanne na magari tano ya kijeshi kuharibiwa, kaskazini magharibi mwa mji wa Kumbo.

Waziri wa ulinzi atembelea maeneo yenye ukosefu wa usalama

Waziri wa ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo ametoa wito kwa raia kushirikiana na jeshi la nchi hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu wapiganaji.

"Ningependa kusisitiza kwamba kuwepo kwetu hapa ni dhihirisho kwamba serikali inafanya kila juhudi kupata suluhu la matatizo ya usalama yanayoendelea kusumbua watu wetu. Tunatambua kwamba watu wa hapa wanaendelea kuomba usalama uimarishwe na utulivu udumu kwa maendeleo ya eneo hili.”

Waziri huyo wa ulinzi ametoa wito kwa wapiga kura na wagombea kutozingatia vitisho vya makundi ya wapiganaji na kuendelea na mchakato wa uchaguzi.

Ametoa wito kwa wakaazi wa sehemu hiyo waliotoroka kurejea makwao.

Matayarisho ya uchaguzi yanaendelea

Serikali imesema kwamba uchaguzi wa Desemba 6 utahakikisha kwamba maslahi ya watu wanaozungumza kiingereza yanatekelezwa namla ilivyokubaliwa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyoitishwa na rais Paul Biya kati ya Septemba 30 na Oktoba 4 mwaka uliopita.

Maeneo yanayoishi watu wanaozungumza kiingereza yaliingia katika machafuko mwaka 2016 wakati walimu na mawakili walipodai kwamba walikuwa wanabaguliwa ilikinganishwa na wenzao wanaozungumza kifaransa.

Serikali ilijibu kwa msako wa kijeshi na kupelekea makundi ya wapiganaji kuchukua sialaha na kuanza vita wakisema kwamba walikuwa wanawalinda raia.

Kulingana na umoja wa mataifa, watu 3,000 wameuawa na zaidi ya nusu milioni kuachwa bila makao kufuatia mapigano hayo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG