Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 22:07

Wapigakura wa Marekani wamezungumza na VOA kuhusu wagombea urais


Wagombea urais Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump

Wapiga kura kote nchini Marekani wamezungumza na Sauti ya Amerika-VOA kuhusu masuala ambayo ni muhimu sana kwao na kuelezea nani wamempigia kura na kwanini.

Maoni yao na mawazo yameonyesha hamasa kubwa ambayo imeambatana mara kwa mara na maoni mchanganyiko. Huko Dearborn, katika jimbo la Michigan, Zahraa Alakashi mzaliwa wa Saudi Arabia alisema alikuwa na wasi wasi mkubwa kuhusu mgombea urais wa Republican, Donald Trump ambaye katika siku zilizopita ametaka wahamiaji wa kiislamu kupigwa marufuku kuingia nchini Marekani.

Alakashi alisema amempigia kura mdemocrat Hillary Clinton. Hii ni mara yangu ya pili kupiga kura, mara ya kwanza ilikuwa kwa Obama, rais wa kwanza mweusi, na mara ya pili nina matumaini ni kwa ajili ya rais wa kwanza mwanamke.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG