Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:39

Wapiga kura Tunisia wajitokeza kwa kiasi kidogo katika uchaguzi wa bunge


Uchaguzi Tunisia
Uchaguzi Tunisia

Uchaguzi unafanyika miaka 12 baada ya muuza mboga Mohamed Bouazizi kujichoma moto mwenyewe katika hatua ya maandamano ambayo yalipelekea machafuko ya kiarabu , uchaguzi huo utakuwa wa bunge jipya ambapo wajumbe wake watakuwa na uwezekano wa kuwa na ushawishi mdogo kwenye sera za serikali.

Idadi ya watu waliojitokeza kwenye chaguzi nyingi zilizopita tangu mapinduzi ya mwaka 2011 ambayo yalitikisa udiktekta na kuleta mabadiliko ya demokrasia ilionekana kuwa juu kuliko siku ya Jumamosi wakati watu wachache wa Tunisia walionekana kwenye vituo vya kupigia kura katika mji mkuu.

Shirika la habari la Reuters limetembelea vituo sita vya kupigia kura kuzunguuka Tunisia ambavyo vilikuwa kimya. Katika kipindi cha masaa mawili katika wilaya za Ettadamon na Ettahir mwandishi wa habari kutoka shirika hilo aliona takriban wapiga kura 20 wakipiga kura zao.

Tume huru ya uchaguzi ambayo wajumbe wake wanateuliwa na Saied wamesema takriban asilimia 3 kati ya wapiga kura milioni 9 wanaoruhusiwa kupiga kura wametekeleza jukumu lao la msingi la kupiga kura majira ya asubuhi Jumamosi.

XS
SM
MD
LG