Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:21

Wapelestina walalamikia makazi kwenye Ukingo wa magharibi


Picha ya sehemu ya Ukingo wa magharibi.
Picha ya sehemu ya Ukingo wa magharibi.

Kundi la wanaharakati dhidi ya ujenzi wa makazi ya kiyahudi limesema kuwa serikali ya Israel Jumapili imetangaza mpango wa kujenga makazi mengine 780 kwenye ukingo wa magharibi ikitarajia uungaji mkono kutoka Marekani katika siku za mwisho za utawala wa Trump.

Kundi hilo linalojulikana kama Peace Now, limesema kuwa asilimia 90 ya majengo mapya yako ndani ya ukingo wa magharibi kwenye eneo ambalo wapalestina wanapanga liwe taifa lao katika miaka ya baadaye. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, inasemekana kuwa zaidi ya nyumba 200 zimejengwa kwenye maeneo yasiokubaliwa na ambayo serikali ya Israel imeamua kuhalalisha.

Peace Now limeongeza kusema kuwa serikali ya Israel imeongeza ujenzi wakati wa utawala wa Trump ikisemekana kuwa zaidi ya nyumba 12,000 ziliidhinishwa kujengwa mwaka uliopita, idadi iliyo kubwa zaidi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu takwimu zilpoanza kuchuliwa mwaka wa 2012.

Kundi hilo limesema kuwa kwa kufanya hivyo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa mara nyingine ameweka maslahi yake ya kisiasa mbele ya maslahi ya taifa. Limeongeza kusema kuwa ujenzi huo unadumaza matumaini ya kupatikana kwa suluhisho la kudumu kati ya Israel na Palestina katika siku za mbele na huenda ukazua uhasama na utawala mpya wa marekani katika siku za karibuni.

Kufikia sasa hakuna majibu yoyote kutoka kwa utawala wa Netanyahu ingawa wiki iliyopita alisema kuwa ataomba kuidhinishwa kwa miradi hiyo ya ujenzi. Miradi hiyo ni pamoja na nyumba 100 kwenye eneo la Tal Menashe ambapo mwanamke mmoja wa Israel aliuwawa mwezi uliopita kwenye shambulizi ambalo mwanaume wa kipalestina ameshitakiwa. Wapalestina wamekuwa wakidai ardhi ya ukanda wa magharibi iliyochukuliwa na Israel katika mapigano ya mwaka 1967.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG