Wizara ya afya ya Palestina imesema wanaume watatu waliuawa wakati wa shambulio huko Balata, ambako kuna kambi ya wakimbizi karibu na mji wa Nablus. Watu sita walijeruhiwa, akiwemo mtu mmoja ambaye yuko katika hali mahututi, wizara hiyo imesema.
Jeshi la Israel lilithibitisha baadaye kwamba wanajeshi walilishambulia eneo la Balata. Limesema wanajeshi walishambuliwa kwa risasi na waliwaua Wapalestina watatu.
Jeshi limeongeza kuwa watu wengine watatu walikamatwa.
Hata hivyo, utawala wa Biden ulitoa taarifa yenye maneno makali Jumapili, ukiikosoa Israel kwa kuendelea kuweka tena makazi ya walowezi katika kituo cha zamani cha Homesh kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.