Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:49

Wapalestina sita wameuawa katika operesheni ya Israel


Mwanafunzi wa Palestina akikimbia baada ya maafisa wa usalama wa Israel kurusha gesi ya kutoa machozi wakati wa makabiliano ya Agosti 6, 2022

Msemaji wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Nabil Abu Rudeineh, ameishutumu Israel kuhusiana na vifo vya wapalestina sita, akiwemo kiongozi wa kundi la wapiganaji wa kijeshi, waliouawa katika mapambano na wanajeshi wa Israel.

Mapambano hayo yametokea wakati wa operesheni ya kijeshi katika mji wa Nablus, huko ukingo wa Magharibi.

"Mashambulizi ya Israel yamevuka mipaka yote iliyowekwa kati yake na Palestina. Wanajeshi wa Israel wameua watu sita katika muda wa saa 12, katika mji wa Nablus na tunatoa wito kwa uongozi wa Marekani kuishinkiza serikali ya Israel kuacha mapigano. Mauaji haya ya kila siku yanayotekelezwa na jeshi la Israel ndio yanayochochea mapambano na utawala wa Marekani unastahili kuchukua hatua kwa haraka kabla ya hali kuharibika zaidi," amesema msemaji wa rais wa Palestina, Mahmoud Abbas.

Waziri mkuu wa Israel Yair Lapid amewasifu wanajeshi wake na kuahidi kwamba ataendelea kuwasaka wanaoishambulia Israel.

Amesema kwamba Israel haitaruhusu kuwepo kwa makundi ya kigaidi yanayotishia maisha ya watu wa Israel na wanajeshi wake.

"Baada ya msako wa usiku, nataka kusema kwamba lengo letu ni kuwapiga vilivyo magaidi na wanaowatuma katika miji ya Jenin na Nablus na kwingineko ambako ugaidi unaota mizizi. Hatutachoka hata kidogo. Kuuawa kwa Waddia Al-Houh, kiongozi wa kundi la Lion's Den, pamoja na magaidi wengine ni matokeo ya operesheni ya pamoja ya maafisa wa usalama, mamlaka ya usalama ya Israel na idara ya kupambana na ugaidi ya Israel katika mji wa Nablus."

Zaidi ya Wapalestina 100 wameuawa huko Ukingo wa Magharibi mwaka huu.

Mashambulizi ya mitaani yanayotekelezwa na wapalestina, yameua watu 20 katika sehemu zinazokaliwa na Waisrael na wapalestina.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG