Wizara ya afya ya Gaza pamoja na chombo cha habari cha serikali ya Hamas wamesema kuwa shambulizi hilo limetokea kwenye moja wapo ya maeneo yenye watu wengi waliokoseshwa makazi, na kwamba zaidi ya wengine 100 wamejeruhiwa.
Jeshi la Israel limesema kuwa lililenga kamandi inayodhibitiwa na Hamas ndani ya shule hiyo iliyopo kati kati mwa Gaza. Taarifa zimeongeza kusema kuwa shule hiyo ilikuwa ikitumika kurushia silaha dhidi ya vikosi vya Israel, pamoja na hifadhi ya silaha, na kwamba ilani ilitolewa kwa raia kabla ya kufanywa kwa shambulizi hilo.
Kwenye mashambulizi ya awali sawa na hilo, jeshi la Israel limekuwa likilaumu kundi la Hamas, kwa kuweka raia kwenye hatari, na kufanyia operesheni zake kwenye maeneo yenye misongamano mikubwa ya watu kama shule na hospitali, dai ambalo kundi la Hamas limekanusha.
Maafisa wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanalaumu Israel kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwenye mapigano hayo bila kuhakikisha kuwa raia wana mahala salama pa kutorokea. Maafisa wa Israel wanakisia kuwa takriban wapiganaji 14,000 wa Hamas na Islamic Jihad, wameuwawa au kuzuiliwa, wakiwa miongoni mwa wapiganaji takriban 25,000 waliokuwepo wakati vita hivyo vikianza.
Forum