Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 06:06

Waongoza ndege JKIA walaumiwa kwa kumpotosha rubani


Waongozaji ndege katika Uwanja wa ndege wa Wilson wanaamini kuwa rubani wa ndege iliyoanguka katika milima ya Aberdare wiki iliyopita nchini Kenya, na kuuwa watu wote kumi alipotoshwa na waongozaji ndege waliokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi.

Kosa hilo, ambalo linajulikana katika duru za wanaanga kama kuendesha ndege katika eneo lenye kizuizi (CFIT) linatokea pale ambapo ndege inayokidhi kiwango cha kuruhusiwa kuruka, ikiwa inaelekezwa na rubani mwenyewe, ikianguka kutokana na kuwepo mawasiliano mabaya kutoka kituo cha kuongoza ndege.

Wachunguzi walitazamiwa kurudi katika eneo la ajali huko Njabini kukusanya mabaki ya ndege hiyo kwenye eneo lenye mawe wakati timu nyingine inafungua vinasa sauti vilivyoko katika kituo cha kuongoza ndege huko JKIA. Yale ambayo yatabainika na timu mbili hizo yanaweza kutoa mwanga zaidi juu ya madai ya timu ya Wilson kuhusu ajali hiyo.

Ndege hiyo yenye umri wa miaka 22 ilikuwa inasafiri kuelekea Nairobi ikitokea Kitale Jumanne iliyopita ilipoanguka katika milima hiyo majira ya saa kumi na moja jioni kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya, na abiria wanane na wafanyakazi wawili kupoteza maisha.

Gazeti la The Nation limethibisha kuwa Rubani Barbara Wangeci, 28, alituma ujumbe wa radio katika kituo cha kuongoza ndege na walimshauri atue JKIA, upande wa eneo la Utawala.

Lakini, rubani huyo alikuwa hana uzoefu na eneo hilo kwani siku zote akitua katika Uwanja wa ndege wa Wilson, na kwa hivyo Kituo cha kuongoza ndege cha JKIA kiliahidi kumsaidia kumwelekeza kuondoka kutoka msitu wa Aberdare ili aelekee sehemu ya eneo maalum la Avena, na aendelee kuruka kuelekea uwanja wa JKIA, ambapo alikuwa atue katika njia ya ndege nambari 24.

Wangeci alikuwa ameruka umbali wa futi 11,000 wakati alipogeuza ndege na kuelekea mlimani kama alivyopewa maelekezo. Satima, eneo la juu kabisa la mlima wa Aberdares, ulikuwa mbele yake katika mnyanyuko wa futi 13,120, wakati Mlima wa Elephant, ambako ndege ilianguka ulikuwa katika muinuko wa futi 12, 815 mbele yake. Kutokana na ukungu ulikuwa umemziba kuona, Wangeci hakutambua kuwa alikuwa anaipeleka ndege kwenye kizuizi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG