Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:04

Wanawake waukumbuka mwaka 2016 ni wenye changamoto nyingi


Wanawake kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi washiriki katika maandamano ya mwanamke duniani Nairobi, Kenya 2015.
Wanawake kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi washiriki katika maandamano ya mwanamke duniani Nairobi, Kenya 2015.

Wanawake wa Marekani wanahisi uteuzi wa Hillary Clinton kuwania urais umefungua njia kwa wanawake wengi zaidi kujitoma katika ulingo wa siasa na kuwania nafasi za juu za uongozi.

Mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wa matukio mengi kwa upande wa wanawake hapa Markekani na huko barani Afrika.

Marekani ilishuhudia wanawake wakiweka historia katika medani ya siasa pale chama cha Demokratik kilipomteua rasmi, Hillary Rodham Clinton mwanasiasa mwanamke kuwa mgombea urais katika uchaguzi ambao ulifanyika Novemba 8.

Mwanamke huyu anakumbukwa na wengi siyo tu kwa vile yuko katika ulingo wa siasa, bali wengi wanamkumbuka kuwa ni mwanamke ambaye hajawahi kusahau kule alikotoka au anampigania nani katika maisha yake yote.

Mchango wa Hillary utakumbukwa kila mahali kwa msimamo wake wa kiliberali katika masuala ya kijamii, kuunga mkono haki za wanawake kutoa mimba, usawa katika ndoa, na pia mageuzi ya uhamiaji miongoni mwa masuala mengi ambayo amekuwa akiyazungumzia.

Na huko barani Afrika mengi yametokea na kubainisha kuwa safari ya kuleta maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kielimu na kijamii bado yanaendelea na yatatawala tena kwa mwaka ujao wa 2017.

Hillary Clinton
Hillary Clinton

Wakati wanawake wa Tanzania wamefanya tathmini ya serikali inavyozingatia usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu hususan katika kumkomboa mwanamke, nchini Kenya mwaka huu ulishuhudia suala utekelezaji wa katiba na masuala ya afya kama yanavyomkabili mwanamke wa Kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:18:11 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

DRC wanawake waliendelea kulalamikia ukosefu wa usalama hasa kwa wanawake wanaoishi maeneo ya mashariki mwa nchi na hivyo kugubikwa na ghasia na vurugu ambazo hazijulikani hatima yake.

Lakini licha ya yote haya ambayo yanatokea kote duniani na barani Afrika yanayowahusu wanawake , mwezi Januari katika mkutano uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia ulizungumzia changamoto sabab ambazo zinawakabili wanawake wa Afrika.

Changamoto hizo zilitajwa kuwa ni kutengwa kiuchumi, ukosefu wa fursa za elimu kwa wasichana, ghasia za kijinsia, mila potofu, kutengwa kisiasa na katika maisha ya umma, kuwekwa kando katika mezaz za mazungumzo kuhusu amani.

XS
SM
MD
LG