Kufuatia ukamatwaji huo, baraza la mahakama ya Florida imerejesha hati ya mashitaka kwa watu wote 11 sambamba na mashitaka mbalimbali yanayohusiana na mauaji ya Moise akiwa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, hapo Julai 7, 2021.
Mke wa rais huyo wa zamani alifyatuliwa risasi mara kadhaa lakini alipona.
Markenzy Lapointe, mwanasheria wa mahakama ya wilaya ya kusini mwa Florida alitangaza katika mkutano na wanahabari kwamba watuhumiwa wanne wamekamatwa Jumanne.
Aliwatambulisha kwa majina yao ambao ni Arcangel Pretel Ortiz raia wa Colombia na mkazi wa kudumu wa Marekani, Antonia Intriago, mfanyabiashara wa Colombia na mkazi wa kudumu wa Marekani, Walter Veintemilla raia wa Marekani anayetokea Ecuador na kuishi Florida, na Frederick Bergmann raia wa Marekani.