Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:35

Wanawake watatu wapewa Tunzo ya Amani ya Nobel


Washindi wa tunzo ya amani ya Nobel 2011, Tawakul Karman, (kushoto), Leymah Gobwee, na rais Ellen Johnson Sirleaf
Washindi wa tunzo ya amani ya Nobel 2011, Tawakul Karman, (kushoto), Leymah Gobwee, na rais Ellen Johnson Sirleaf

Tunzo mashuhuri ya amani ya Nobel kwa mwaka 2011, imetolewa kwa wanawake watatu kwa juhudi zao za kutetea haki za wanawake na kuleta amani.

Ikitangaza habari hizo, kamati ya Nobel ya Norway mjini Oslo imeeleza kwamba, wanawake hao watatu wanapewa heshima hiyo kutokana na vita vyao vya kutotumia nguvu kwa ajili ya usalama wa wanawake na haki za wanawake.

Mwenyekiti wa kamati Thorbjoern Jagland alisema, ni matumaini kwamba zawadi itawasdia kuhamasisha watu kufahamu masuala ya wanawake kote duniani.

“Ni matumaini ya kamati ya nobel ya Norway kwamba zawadi kwa Ellen Johnson Sirleaf, Leymah Gbowee na Tawakkul Karman, itasaidia kufikisha kikomo ukandamizaji wa wanawake unaoendelea katika mataifa mengi, na kutambua uwezo mkubwa kwa ajili ya demokrasia na amani walonao wanawake”.

Ellen Johnson Sirleaf mewnye umri wa miaka 72 ni mwanamke wa kwanza Afrika kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia kuwa rais 2005. Kamati imesifu juhudi zake za kudumisha amani, kuhamasisha maendeleo ya uchumi na jamii na kuimarisha hadhi ya wanawake nchini Liberia.

Rais Ellen Johnson Sirleaf na rais Barack Obama
Rais Ellen Johnson Sirleaf na rais Barack Obama

Akizungumza na sauti ya amerika mjini Monrovia Bi Sirleaf alisema amefarijika kupokea tunzo kwa niaba ya wanawake wote wa Liberia.

“Nimefurahi sana, ninashukuru, kwa heshima na taadhima kukabidhiwa zawadi hii. Ninaamini ni kwa ajili ya kutaambua miaka mingi ya mapambano. Lakini pia ninamini ni kutambua hamu ya walibera kutafuta amani. Na ukweli ni kwamba mnamo miaka minane wameweza kwa pamoja kudumisha amani”.

Leymah Gobwee
Leymah Gobwee

Mshindi mwengine wa tunzo hiyo Leymah Gbowee mwenye umri wa miaka 39 kutoka Liberia ameisaidia nchi yake kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe kuwahamasisha wanawake wa kikristo na waislamu kushiriki pamoja katika mlolongo wa mandamano ya amani bila ya kutumia ghasia.

Nae Tawakkul Karman mwenye umri wa miaka 32 ni mwanaharakati na mwandishi habari wa yemen aliyesifiwa kwa jukumu lake la uwongozi katika vita vya kupigania haki za wanawake, demokrasia na amani nchini mwake, juhudi zilizoharibiwa kutokana na maandamano na ghasia za mwaka huu.

Waandishi habari walimkuta Karman hii leo mahala ambapo amekuwa akifika kila siku kwa miezi minane sasakatika hema ya malalamiko katika mji mkuu wa sanaa.

“Tunzo ya nobel ni ya wanamapinduzi wa amani kote katika nchi za kiarabu na wananchi wa yemen pamoja na wale walouwawaau kujeruhiwa katika juhudi zao za kupatikana amani”.

Wanawake hao watatu watagawanya zawadi ya amani ya dola milioni 1.5 itakayotolewa oslo Disemba 10, 2011.

XS
SM
MD
LG