Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:14

Wanawake wawili mashuhuri watangaza rasmi kuwania urais Ufaransa


Mmoja wa wagombea wa urais Ufansa Marine Le Pen
Mmoja wa wagombea wa urais Ufansa Marine Le Pen

Wanasiasa wawili wanawake mashuhuri wa Ufaransa Jumapili wamezindua kampeni zao kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa  kufanyika mwaka ujao.

Marine le Pen kutoka;chama cha National Rally chenye msimamo wa kulia pamoja na meya wa Paris ambaye ni msocialisti Anne Hidalgo, sasa wamejitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro;hicho.;

Hidalgo mwenye umri wa miaka 62, ambaye amekuwa meya wa Paris tangu 2014 ana uwezekano mkubwa wa kushinda uteuzi wa chama cha Socialist huku akisema kwamba angependa kuona watoto wote nchini Ufaransa wakipata nafasi sawa na alizopata yeye katika maisha yake kama mtoto wa wahamiaji kutoka Uhispania.

LePen mwenye umri wa miaka 53 kwa upande wake ameanzisha kampeni kwenye mji wa kusini wa Frejus wakati akiahidi kulinda uhuru wa Ufaransa. Wawili hao sasa wanaingia kwenye orodha kubwa ya wagombea akiwemo rais wa sasa ,menye msimamo wa wastani Emmanuel Macron.

Macron mwenye umri wa miaka 43 bado hajatangaza nia yake ya kuwania urais, ingawa anatarajiwa kufanya hivyo hivi karibuni. Ushindani mkubwa kwenye zoezi hilo unatarajiwa kuwa kati ya Le Pen na Macron sawa na ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa rais wa 2017.

XS
SM
MD
LG