Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:30

Wanawake waliotekwa Burkina Faso ni 50


Takriban wanawake 50 wametekwa nchini Burkina Faso na wenye msimamo mkali wa Islamic State katika eneo la Sahel, kaskazini mwa Burkina Faso wiki iliyopoita kwa mujibu wa maafisa wa huko waliozungumza Jumatatu.

Utekaji huo ulitokea Januari 12 na 13, takriban kilometa 15 kutoka Arbinda katika jimbo la Soum, alisema lutein kanali Rodolphe Sorgho ambaye ni gavana wa Sahel, katika taarifa yake.

Wanawake walitekwa walipokuwa nje wakichuma matunda nje ya mji alisema.

Ghasia za kijihadi zinazo husishwa na kundi la Al Qaida na Islamic State zimegubika Burkina Faso, na kusababisha mauaji ya maelfu yawatu na kukosesha makazi watu milioni 2 katika taifa hilo la Afrika magharibi.

Kushindwa kwa serekali kuzuia mapigano kumesababisha hali kutokuwa na utulivu na kusababisha mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka 2022.

XS
SM
MD
LG