Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:40

Wanawake wa Uganda wadai haki za wajawazito


Wakinamama wajawazito katika hospitali moja katika kijiji cha Iganga kaskazini ya Uganda
Wakinamama wajawazito katika hospitali moja katika kijiji cha Iganga kaskazini ya Uganda

Wanaharakati wa kutetea haki za wajawazito wanaitaka mahakama ya kikatiba itangaze kuwa mama kufariki akijifungua ni ukikwaji wa haki zake.

Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya, takriban wanawake kumi na sita hufariki kila siku wakijifungua, nchini Uganda. Kutokana na hali hiyo wanawake wakiongozwa na takriban wanaharakati mia moja wa kutetea haki za wamama wajawazito walifanya maandamano ya amani na kutembea kilomita tano kutoka ofisini mwao na kwenda kwenye mahakama ya katiba.

Nakibuuka Nuru Musisi kando na kuwa mja mzito, ni mwanaharakati wa kutetea haki za wamama wajawazito.

Anasema wamefika mahakamani kwa sababu " Tunataitaka serikali itangaze kuwa wamama kufariki wakiwa hospitalini ni ukiukwaji wa haki zao za kuishii na afya bora. Pili, tuliwasisilisha malalamiko yetu kwenye mahakama ya kikatiba miezi saba iliopita na kufikia sasa hatujapata jibu lolote. Tunaiuliza mahakama itoe msimamo kuhusu suala hilo.

Wanaharakati wa kutetea haki za wamama wajawazito wanaitaka serikali kuwaajiri wakunga na madaktari wa kuwahudumia wamama wajawazito. Sio jambo la kushangaza kumuona mkunga mmoja akiwahudumia zaidi ya wamama hamsini kila siku. Wanasema kesi nyingi za wamama wanaofariki wanafariki kwa sababu hawakupata usaidizi unaofaa kwa wakati unaofaa.

Ingawa sheria inasema mama mjamzito akienda kwenye hospitali ya serikali hafai kulipishwa pesa zozote wala kuitishwa kitu chochote cha matumizi anapojifungua, hali ilivyo sasa ni kwamba mama mjamzito akienda kwenye hospitali hizi za serikali kujifungua, hulazimishwa kununua kila kitu atakachotumia kama vile pamba, wembe, makasi na vinginevyo.

Miezi saba wakati wanaharakati wa kutetea haki za wamama wajawazito walipowasilisha malalamiko yao kwenye mahakama ya kitaba wakitaka serikali iwajibike ikiwa mama mja mzito atayapoteza maisha yake,

"Mkuu wa sheria alilipiga ombi letu akisema hili ni suala la sera za serikali na mahakama haina uwezo wa kuamua suala kama hilo. Sisi kama wanaharakati tunasema malalamiko yetu yanagusia maswala ya haki za binadamu. Hatutaki sera za serikali zibadilishwe lakini tunataka itangazwe kuwa wamama kufariki wakiwa hospitalini ni ukuikaji wa haki zao za kuishi na afya."

Baada ya kuyapokea malalamiko yao, msajili wa mahakama ya kikatiba Erias Kisauzi alisema mkuu wa sheria ana haki ya kutoa maoni yake huku akisisitiza kuwa mahakama itatilia maanani ombi na wamama

"Tunaomba msamaha kwa niaba ya mahakama na ninawahakikishia kuwa nitalifuatilia suala hili. Malalamiko yenu yamesikika na mtaupata uamuzi wa kesi yenu hivi karibuni. Naweza kusema hivi karubuni na hivi karubuni itakuwa hivi karibuni."

Huku Waganda wengi wakilalamika kuhusu hali duni ya huduma za afya wanazopata kwenye hospitali za serikali, Wizara ya fedha inapanga kupugunguza bajeti ya wizara ya afya kwa asili mia sita kwenye bajeti ya mwaka wa 2012/2013.

XS
SM
MD
LG