Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:01

Wanawake wa Sudan Kusini wanapatiwa mafunzo ya kazi za mikono


Wanawake wa Sudan kusini wakijifunza kutengeneza kazi za mikono mjini Juba.
Wanawake wa Sudan kusini wakijifunza kutengeneza kazi za mikono mjini Juba.

Kundi la wanawake kutoka mkoa wa Greater Equatorial huko nchini Sudan Kusini linawapatia mafunzo darzeni ya wanawake wengine jinsi ya kutengeneza bidhaa za mikono kusudi waweze kuziuza na kujipatia fedha za kujikimu kimaisha.

Wanawake vijana 30 wanajifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa za mikoba, vipochi na vitambaa vya meza kutokana na vifaa vya ndani ya nchi kama vile shanga. Maafisa katika taasisi ya Women Advance mjini Juba ambayo imeandaa mafunzo hayo walisema wanaamini kuwa mbinu mpya siyo tu zitawawezesha wanawake kujipatia fedha lakini pia zitafungua milango ya ajira kwa wanawake wengine.

Wanawake wanatarajiwa kutumia muda wa wiki mbili kujifunza jinsi ya kutengeneza vifaa hivyo. Munira Michael ambaye amekuwa akiuza chana kwenye soko moja mjini humo amejifunza jinsi ya kutengeneza vitambaa vya meza na kwa uso wa tabasamu alisema amepata ujuzi wenye faida utakaomuongezea kipato.

XS
SM
MD
LG