Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:11

Wanawake na wasichana wa Afghanistan wataabika baada ya tetemeko la ardhi


Wanawake na wasichana wako katika hali mbaya na hatari Afghanistan, kufuatia matetemeko ya ardhi ya hivi karibuni kwa sababu ya migogoro ya kibinadamu na haki za kiraia tangu Taliban kutwaa mamlaka, afisa wa Umoja wa Mataifa amesema Jumapili.

Taarifa kutoka idara ya Umoja wa Mataifa ya wanawake ilieleza baadhi ya matatizo ambayo wanawake wanakumbana nayo katika maeneo ya jimbo la Herat, ambako mfululizo wa matetemeko ya ardhi mwezi huu yaliua maelfu ya watu, zaidi ya asilimia 90 ya hao walikuwa wanawake na watoto, na kuharibu karibu kila nyumba.

Desturi za kitamaduni hufanya isiwezekane kwa wanawake kukaa hema moja na majirani au familia zingine, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.

Wanawake wengi pia wana shida kupata misaada ya kibinadamu ikiwa hawana jamaa wa kiume ambaye anaweza kuipata kwa niaba yao na kukosekana kwa vituo vya kusambaza misaada ya wafanyikazi wanawake, Umoja wa Mataifa umesema.

Forum

XS
SM
MD
LG