Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:43

Wanasiasa waliokamatwa nchini Kenya wanatafuta njia za kupatiwa dhamana


Wanasiasa wa upinzani Kenya kutoka (L) Florence Mutua, Junet Mohammed, Ferdinand Waititu na Moses Kuria
Wanasiasa wa upinzani Kenya kutoka (L) Florence Mutua, Junet Mohammed, Ferdinand Waititu na Moses Kuria

Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya ambao walifikishwa mahakamani siku ya Jumanne kwa shutuma za kutoa matamshi ya kuchochea chuki, Jumatano waliwasilisha maombi ya kuachiliwa kwa dhamana mbele ya mahakama kuu.

Wanasiasa wa upinzani
Wanasiasa wa upinzani

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, wanasiasa hao watano na mwanafunzi wa chuo kikuu walikamatwa Jumanne na kuamriwa na jaji wa mahakama ya Milimani mjini Nairobi na kuwekwa katika rumande ya polisi hadi siku ya Ijumaa ili kuwapa viongozi wa mashtaka muda wa kutosha kufanya uchunguzi.

Washukiwa hao walifikishwa mahakamani pamoja na wanasiasa wengine wanaoegemea mrengo wa kisiasa wa Jubilee baada ya baadhi yao kukamatwa kutoka majumbani mwao na wengine kwenda wenyewe polisi na kufunguliwa mashtaka.

Kwa mujibu wa gazeti hilo la Daily Nation liliwanukuu wanasiasa hao wakisema kuwa wameshikiliwa kwa muda wa saa kumi na nane bila kupatiwa huduma ya chakula, maji wala matibabu.

XS
SM
MD
LG