Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:38

Wanasiasa wa Mali wako tayari kushirikiana na serikali ya mpito.


Cheick Traore ni kiongozi wa chama cha kisiasa cha African Convergence for Renewal (CARE).
Cheick Traore ni kiongozi wa chama cha kisiasa cha African Convergence for Renewal (CARE).

Raia wa Mali wanataka kurejea katika maisha yao ya kawaida na mwanasiasa maarufu nchini humo anadai wanataka kushirikiana na serikali ya mpito.

Mwanasiasa mmoja maarufu nchini Mali anasema anaamini vyama vingi vya siasa vitafanya kazi na serikali mpya ya mpito wakati nchi hiyo ikijiandaa kumwapisha rais wa muda.

Cheick Traore kiongozi wa African Convergence for Renewal Party aliiambia Sauti ya Amerika kuwa raia wa Mali wanataka kurejea kwenye maisha ya kawaida ya kikatiba.

Amesema “itabidi tufanye kazi na serikali ya mpito kwasababu wote tunachotaka leo ni usalama nchini humu. Pia tunataka uchaguzi uandaliwe ili tuweze kuwa na rais mpya wa kuchaguliwa”

Spika wa bunge la Mali Dioncounda Traore anatarajiwa kuapishwa alhamisi na atakuwa na siku 40 kwa mujibu wa katiba kuandaa uchaguzi mpya.

Kipindi cha mpito ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita kati ya jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi (ECOWAS) na wanajeshi waasi wa Mali ambao walimtoa madarakani rais Amadou Toumani Toure.

Cheick Traore alionya kwamba jeshi linajiweka pembeni na watu waelewe kwamba bado litahusika katika kuhakikisha kwamba kipindi cha mpito kinakwenda salama.

XS
SM
MD
LG