Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 13:27

Wanasheria, wanasiasa washinikiza kamera ziruhusiwe ndani ya chumba cha mahakama kwenye kesi za Trump


Rais wa zamani Donald Trump akipunga mkono kabla ya kupanda ndege yake ya kibinafsi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, Jumanne, Juni 13, 2023. AP.
Rais wa zamani Donald Trump akipunga mkono kabla ya kupanda ndege yake ya kibinafsi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, Jumanne, Juni 13, 2023. AP.

Wakili wa Trump John Lauro alisema angependelea kesi ionyeshwe kwenye runinga lakini alisisitiza kuwa hayo yalikuwa maoni yake binafsi

Wito unazidi kuongezeka kwa kesi za jinai za Donald Trump kutangazwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari huku Marekani ikikabiliana na matarajio ya kumuona rais wa zamani na pengine baadaye akiwa kizimbani.

Wanasheria na wanasiasa wanajitokeza kushinikiza kamera ziruhusiwe ndani ya chumba cha mahakama haswa wakati rais huyo wa zamani ambaye pia ni nyota wa TV za Reality anapokabiliana na mahakama kwa madai kwamba alijaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Kwa kuzingatia hali ya kihistoria ya mashtaka yaliyoletwa katika kesi hizi ni vigumu kufikiria hali ya nguvu zaidi ya kesi zinazoonyeshwa kwenye televisheni ilieleza barua iliyotiwa saini Alhamisi na mbunge wa California Adam Schiff na wenzake kadhaa wa Chama cha Democrat.

Ikiwa umma utapokea matokeo kamili itakuwa muhimu sana kwao kushuhudia moja kwa moja iwezekanavyo jinsi kesi zinavyoendeshwa nguvu ya ushahidi uliotolewa na uaminifu wa mashahidi, barua hiyo ilisema.

Wakili wa Trump John Lauro alisema angependelea kesi isikilizwe kwenye runinga lakini katika shoo kadhaa za TV siku ya Jumapili alisisitiza kuwa hayo yalikuwa maoni yake binafsi.

Forum

XS
SM
MD
LG