Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:18

Wanane wahukumiwa kifungo cha maisha kwa kufanya ugaidi Ivory Coast


Baadhi ya washukiwa wa ugaidi wakiwa mahakamani.
Baadhi ya washukiwa wa ugaidi wakiwa mahakamani.

Mahakama nchini Ivory Coast siku ya Jumatano iliwahukumu kifungo cha maisha wanaume wanne wa Mali waliopatikana na hatia ya kusaidia shambulio la jihadi kwenye eneo la mapumziko la ufukweni na kusababisha vifo vya watu 19.

Mahakama ya Abidjan, katika jiji la biashara, iliwakuta watu hao wanne na hatia kwa makosa waliyoshtakiwa na kuwahukumu kifungo cha maisha, Jaji Charles Bini alitangaza. Shambulio la Machi 13, 2016, lilikuwa la kwanza la wanajihadi kutokea Ivory Coast, moja ya nchi zenye nguvu za kiuchumi za Afrika Magharibi.

Katika operesheni iliyolenga mauaji ya jihadi mwaka uliopita nchini Tunisia, wanaume watatu waliokuwa na bunduki za kivita walivamia ufukwe wa Grand-Bassam, eneo la mapumziko kiasi cha kilomita 40 mashariki mwa Abidjan maarufu kwa raia wa Ulaya, kabla ya kushambulia mahoteli na mikahawa.

Shambulizi la dakika 45 lilimalizika baada ya vikosi vya usalama vya Ivory Coast kuwapiga risasi na kuwaua washambuliaji.

Vifo 19 vilijumuisha raia tisa wa Ivory Coast, wanne wa Ufaransa, na raia mmoja wa Lebanon, Ujerumani, Masedonia, Mali, Nigeria na mtu ambaye hakuweza kutambuliwa, juku watu 33 wa mataifa mbalimbali walijeruhiwa.

Washirika Al-Qaida wa Afrika Kaskazini, na al-Qaida huko Afrika Magharibi (AQIM), sikhu hiyo hiyo walidai kuhusika. Walisema shambulio hilo lilikuwa ni kujibu dhidi ya opeesheni za jihadi katika eneo la Sahel zinazofanywa na Ufaransa na washirika wake, na ziliilenga Ivory Coast kwa kuwakabidhi kwa Mali wahusika wa AQIM.

Watu kadhaa walikamatwa baadaye wakiwemo washukiwa watatu waliouawa ambao walizuiliwa nchini Mali.

18 walishtakiwa Ivory Coast kwa vitendo vya ugaidi, mauaji, jaribio la mauaji, kuficha uhalifu, kumiliki silaha kinyume cha sheria na risasi na kushiriki katika vitendo hivyo, alisema mwendesha mashtaka wa umma, Richard Adou.

XS
SM
MD
LG