Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:31

Wananchi wataka ukweli wa kuvamiwa kituo cha Stakishari


Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania Ernest Mangu
Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania Ernest Mangu

Uvamizi wa vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania umezusha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi nchini humo huku wengine wakipendekeza kuangalia mfumo mzima wa usalama nchini humo ili kurudisha matumaini ya kuwepo kwa amani.

Ripoti ya Dina Chahali wa Dar Es Salaam, Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Matukio kadhaa ya kuvamiwa vituo vya polisi yaliripotiwa sehemu mbalimbali nchini humo kubwa zaidi likiwa la usiku wa kuamkia Jumatatu katika kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Segerea jijini Dar Es Salaam ambapo askari wanne na raia watatu waliuwawa huku majambazi wakiondoka na kiasi kikubwa cha silaha ambazo idadi yake haijajulikana mpaka sasa

Baadhi ya wakazi wa jiji hilo waliozungumza na Sauti ya Amerika-VOA walikuwa na maoni mbalimbali huku wakitoa wito kwa jeshi la polisi kujitathmni katika utendaji wake wa kazi.

Wakati huo huo kamanda wa polis kanda maalum ya Dar Es Salaam bwana Suleiman Kova aliwataka watanzania kuacha kulaumiana kwa wakati huu na kushirikiana kutafuta watu wanaotaka kuvunja amani ya nchi

Naye mkuu wa jeshi la polisi nchini bwana Ernest Mangu pia alitangaza donge nono la shilingi milioni 50 kwa watakaokuwa tayari kutoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa waliohusika na tukio hilo la uvamizi wa kituo cha polisi cha Stakishari

Uvamizi wa kituo cha Stakishari umekuja baada ya hivi karibuni kituo cha polisi wilayani mkuranga katika mkoani Pwani kuvamiwa na kisha askari kadhaa kuuwawa pamoja na kunyang’anywa silaha..

XS
SM
MD
LG