Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:00

Wanamuziki wa Modern Taarab kuzikwa jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waathiriwa wa ajali ya basi iliyosababisha vifo vya wasanii 13 wa Five Stars Moden Taarab, wakisubiri kuwasili kwa maiti mjini Dar es Salaam kutoka Morogoro
Baadhi ya waathiriwa wa ajali ya basi iliyosababisha vifo vya wasanii 13 wa Five Stars Moden Taarab, wakisubiri kuwasili kwa maiti mjini Dar es Salaam kutoka Morogoro

Wanamuziki 13 wa kundi la Five Star's Modern Taarabu waliokufa katika ajali ya gari Morogoro wanatarajiwa kuzikwa jijini Dar es salaam.

Wasanii 13 waimbaji wa mitindo ya taarabu kutoka bendi ya “Five star’s modern taarab” waliokufa kwenye ajali ya gari , wanatarajiwa kuzikwa jijini Dar es salaam baada ya miili yao kusafirishwa kutoka mkoani Morogoro ilikotokea ajali hiyo kuelekea Dar es salaam.

Ajali hiyo ilitokea jumatatu majira ya saa mbili usiku huko Mikumi mkoani Morogoro.

Rais wa bendi hiyo ya Five star’s modern taarab bwana Ali Juma alinusurika katika ajali hiyo, anasema kundi lake lilikuwa linatoka katika ziara ya kimuziki kwenye mikoa ya nyanda za juu.

Bwana Juma amesema dereva wa gari lao aina ya Costa alikuwa mwendo kasi na ghafla aliona gari kubwa aina ya lori mbele yake likiwa limeegeshwa ndipo aliposhindwa kufunga breki na kuligonga gari hilo kwa nyuma.

Aidha amesema watu 12 walikufa papo hapo na mwingine mmoja alifia hospitali. Amesema kundi lake limepoteza vyombo muhimu, ndugu, na marafiki, pigo ambalo haliwezi kusahaulika.

Wakati huo huo kamanda wa polisi mkoani Morogoro bi Adolphina Chialo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG